PATULOUS LITERATURE COMMUNITY
 
HomeHome  RegisterRegister  Log inLog in  MemberlistMemberlist  PublicationsPublications  FAQFAQ  UsergroupsUsergroups  
Hello dear, welcome to JO AFRICA PLC (Patulous Literature Community), we are glad and very delighted to see you here. It's our pleasure to long for your patronage. Register or login into your account for an uninterrupted premium access to our forums. We are honored to have in stock; a lifetime package of the most juiciest and spiciest poems and stories to quench your literary thirst. Hope you won't mind sharing with us what's on your mind. The forum is all yours! We thank you.
ADMIN’S BIOGRAPHY

Jonathan Tafreg (1985-) is a Tanzanian poet, novelist, playwright and a linguist. He is also a professional educator, businessman and a webmaster. He hosts JO AFRICA, an online forum which connects young modern African writers and provides mostly educational and entertaining posts for fans, students and teachers pursuing literature as a course of study or hobby.

He is a strong believer in his own school of thought "Tafregism" which holds that: True life is achieved when truth dominates human life, and that when lies overshadows life, then life becomes counterfeit and meaningless. Some of his quotes and poems can be retrieved from poemhunter.com which is one of the major world's poetry archive.

He is now serving as the head of languages department in one of the leading schools in the country, and has authored several books, composed several poems and recorded tens of tracks since his exposure to the music industry and the writing world in 2007.

He is a self sponsored self promoter who will stop at nothing when it comes to business and creativity. He is now working on his masterpiece "The House of Broken Hearts", a portrayal of magical realism and time travel. Aside from his writing career and web business, Tafreg is a loving husband and a father, currently residing in the Lake Zone, United Republic of Tanzania.

For business dealings, he can be contacted though: spicypoems@gmail.com or by sending him a private message on his website; but he can be also reached directly via +255759988648.

QUICK LINKS:

Share | 
 

 VITA VYA KIMILA

Go down 
AuthorMessage
Jo Africa
Admin
Admin
avatar

Join date : 2017-03-07
Date of Birth : 1985-10-04
Age : 32
Gender : Male Location : Dar es Salaam
Posts : 116
Points : 2505
Work : English Teacher
Talents : Poet, Writer, Singer

PostSubject: VITA VYA KIMILA   Mon Aug 06, 2018 11:11 am

UTANGULIZI
Ilikuwa ni ahsubuhi saana, baridi kali na upepo ule wa alfajiri ulikuwa ukivuma, mawimbi yakiwa yanagonga ufukwe wa ziwa na kutoa mlio kama anavyofyonza kambale, mitumbwi iliyokuwa imefungwa kwa ulegevu tayari ilikuwa maili chache ikitapatapa huku na huko majini. Bata maji na ndege wengine walionekana wakiruka na kutua kwenye mitumbwi ile, wachache walionekana wakidonoa na kutoa vitu majini, bila shaka walikuwa wakipata vifungua vinywa vyao. Pembezoni kulikuwa na boti moja kubwa, lenye maandishi "MV. SIBUOR" ambayo kwa wakati wote huo lilionekana likiwa limetawaliwa na ukimya usio wa kawaida. Ghafla ukasikika mluzi mkali kweli, kuashiria jambo flani, na vijana kadhaa wakatoka nje ya ile boti, ikawa yapata saa kumi na moja na dakika kama ishirini hivi, moshi mweusi ukaonekana ukikwea juu hata mawinguni, ndiposa mzee mmoja wa makamo akatoka nje, akiwa ameambatana na wazee wengine kumi, wakiwa wameshikilia ngozi mbichi ya mwana mbuzi, pamoja na kibuyu. Yule mzee kiongozi akatwaa ile ngozi hata majini na kuianika, wala ile ngozi isipate kuzama, ikawa inaelea na mara ikakauka. Kisha akamimina ile damu iliyokuwa kwenye kibuyu, na ngozi ile ikawa nyekundu kama moto, na ndipo wale wengine wakainamisha vichwa vyao, na kusujudu hata chini, nao wakakaa kimya, na baada ya muda mfupi ile ngozi ikawa mtu, nae akasimama, akaitazama nchi, nayo nchi ikawa maji. Basi kelele zikasikika huku na huko, kelele za wafa maji, wale akina mama ambao walikuwa wamewahi ziwani kuteka maji, kufua na kununua mboga kwa wavuvi wote walizama, mitumbwi mingine nayo ikazama, na pakawa giza gafla. Basi wale wazee wakaingia upande wa ndani mwa ile boti, pamoja na vijana wengine na yule mtu, na mlango wa boti ukafunga, isijulikane kinachofanyika nje, nao ukimya ukatawala mle ndani, na hakika pakawa kimya.


Last edited by Jo Africa on Thu Aug 09, 2018 9:12 am; edited 1 time in total
Back to top Go down
Jo Africa
Admin
Admin
avatar

Join date : 2017-03-07
Date of Birth : 1985-10-04
Age : 32
Gender : Male Location : Dar es Salaam
Posts : 116
Points : 2505
Work : English Teacher
Talents : Poet, Writer, Singer

PostSubject: Re: VITA VYA KIMILA   Mon Aug 06, 2018 12:13 pm

SEHEMU YA KWANZA
Kunako saa isiyojulikana, ukimya ukavunjwa, yule mtu aliyetokana na tambiko akasimama na tazama wote waliokuwa mle ndani wakaangua kilio. Kimo chake kilikuwa yapata futi kumi, pande la jitu, miraba ishirini. Sura yake ilionekana ikiwa imejaa ghadhabu, akamkazia yule mzee kiongozi macho, akaamuru apewe kile kibuyu, nae mzee kiongozi hakuwa na budi, bali kumpatia. Basi akakitwaa na kuimimina damu kinywani mwake, hata ikaisha. Nae akapiga nduru, kelele zile zikasikika hata mbingu, nayo boti ikafunuka upande wa juu, na kisha radi ikashuka na kuipiga boti ile, nayo ikasambaratika, asipate kubaki yeyote aliye hai, nalo lile jitu likasimama juu ya maji, huku vipande vya mbao vikiwa vinaelea huku na huko, hata maiti za wale wazee na vijana zisionekane. Hapo ndipo lile jitu likatazama maji, nayo yakamtii, yakazama hata chini, na tazama maiti zile zilikuwa kama zinalala, na samaki, kobe, vyura, kenge, nyoka, mamba na konokono zikabaki zinajitazama kwa mshangao. Akaikazia macho maiti zile, nazo zikawa hai, nao wakainuka na kushukuru. Wakaendelea na safari wasijue wanakoelekea, lakini lile jitu likawa linawaelekeza njia, nae mzee kiongozi akawa anatafsiri lugha ya lile jitu maana alikuwa haneni kwa lugha ya kibinadamu, bali ishara ambazo aliyeweza kuitafsiri ni yule mzee mwenyewe. Wakaendelea kusonga mbele, wakiwa wamezungukwa na maji pande zote, wakawa wanatembea chini kabisa, katika sakafu ya ziwa. Wakasafiri takribani siku sabini, huku maji yakiwa yanawafuata mara tu baada ya kutoa unyayo. Mzee kiongozi akawaambia wenzake washikilie imani zao, maji yasije yakawameza. Basi wakafunga vinywa vyao, nao wakatembea bila kuona mwanga wa jua, mpaka siku ya sabini. Walikuwa wamechoka na wakapitiwa na usingizi, nao wakalala. Maji hayakuwasubiri, wakamezwa.
Back to top Go down
Jo Africa
Admin
Admin
avatar

Join date : 2017-03-07
Date of Birth : 1985-10-04
Age : 32
Gender : Male Location : Dar es Salaam
Posts : 116
Points : 2505
Work : English Teacher
Talents : Poet, Writer, Singer

PostSubject: Re: VITA VYA KIMILA   Thu Aug 09, 2018 9:20 am

SEHEMU YA PILI
Baada ya ukimya uliotawala kwa takribani saa nne, kelele zikasikika juu ya vilindi vya maji, wengine wakiomba msaada, wengine wakisali sala zao za mwisho, wengine wakiendelea kunywa maji, wengine wakikoroma tu wasijue la kufanya. Basi wakazidi kutapatapa, hofu ikiwa imetanda juu ya nyoyo zao, nao hawakuchoka kutetea maisha yao, ziwa nalo likazidi kuchafukwa, nalo likawaadhibu kwa mawimbi mazito, hata wasiweze kuufikia ufukwe, likawasomba mpaka wakafikia kwenye kisiwa kidogo, kisiwa ambacho hakikuwa kikikaliwa na binadamu yeyote. Nao wakafurahi kuwa binadamu wa kwanza kukanyaga pale. Mzee kiongozi akaanza kuhesabu kikosi chake kama kipo kamili. Lakini kuna jambo lilimshangaza, alipokuwa angali akihesabu, ndipo alipogundua lile jitu halipo, akajua tayari safari ndo imeanza. Wengine hata hawakusumbuka kufikiri juu ya kisiwa kile, wala kuwaza juu ya uhai wa kile kiumbe. Wakaendelea kuhema na kuachama, wakiamini wako salama.

Baada ya muda, hali ya utulivu ikarudi, njaa kali ikiwa inatafuna matumbo yao, nao wakavunja matawi ya miti na wakaanza kuvizia samaki pale ufukweni, wasiweze kuona chochote... Gafla wakasikia sauti ya muziki kwa mbali ukipiga mapigo ya kiasili, tena wakajisikia wako nyumbani, mara furaha na tabasamu zikatanda juu ya sura zao, hata wakaanza na kutikisa vichwa vyao, mara mabega, mara miguu, mara mikono, mara viuno, mara mwili mzima ukaanza kucheza. Wakajikuta wakicheza na kusahau habari za njaa na taabu zote walizozipata. Yule mzee kiongozi akawakumbusha wenzake, akawaambia:

"Jamani enh, huo si mziki wa kawaida, acheni kucheza, kwa akili zenu, mnadhani mama zenu wapo huku? Hata mfurahi kama mbwa amfurahiavyo bwana wake anapomletea chakula? Zibeni masikio yenu, fumbeni macho yenu, nanyi mtaweza kusikia na kuona yale yasiyosikika wala kuonekana kwa masikio na macho ya nyama. Vaeni nguo zenu, safisheni akili zenu, kisha mnifuate."

Baada ya kusikia hayo, wale wazee kumi na wawili, pamoja na wale vijana kenda, nao wakavaa nguo zao, nao wakachukua vibuyu vyao, kisha wakamfuata yule mzee kiongozi. Wakateremka hata upande wa pili wa kile kisiwa, nao wakastaajabishwa na yaliyokuwa yakitendeka huko....
Back to top Go down
Sponsored content
PostSubject: Re: VITA VYA KIMILA   

Back to top Go down
 
VITA VYA KIMILA
Back to top 
Page 1 of 1

Permissions in this forum:You cannot reply to topics in this forum
JO AFRICA PLC :: LITERATURE COMMAND POST :: SPICY STORIES-
Jump to: